MWENYEJI WA FAINALI ZA RAGA YA WANAWAKE ATANGAZWA
Jiji la Nairobi litakuwa mwenyeji wa ubingwa wa mwaka huu wa raga ya wanawake barani Afrika kitakachoandaliwa kuanzia tarehe 15 hadi 16 mwezi ujao katika uga wa RFUEA.
Tayari timu zitakazoshiriki zimewekwa kwenye makundi 4 kabla ya kipute hicho ambacho kitaandaliwa nchini kwa mara ya pili baada ya Kenya kuwa mwenyeji wa Makala ya 2014.
Bingwa mtetezi na mshindi wa mashindano hayo mara 12 Afrika Kusini, watamenyana na Zimbabwe na Mauritius katika pool A, huku wenyeji Kenya Lionesses ambao walimaliza wa pili mwaka jana, wamejumuishwa kwenye Pool B wakiwa na Ghana na Ivory Coast.
Pool C inajumuisha Uganda, Zambia na Burkina Faso huku Madagascar, Tunisia na Misri wakiwekwa kwenye Pool D.
Lionesses wanawinda taji la pili kwenye mashindano hayo, baada ya kupoteza dhidi ya Afrika Kusini katika fainali za mwaka jana zilizoandaliwa nchini Ghana.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































