#Sports

FOREST YAWAFUNIKA PORTO, VILLA YAFUNZWA

Klabu ya Nottingham Forest inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza ilipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Porto ya Ureno katika mechi za kuwania ubingwa UEFA UROPA na kumpa meneja Sean Dyche ushindi katika mechi ya kwanza baada ya kuteueliwa.

Forest ambao alimpiga kalamu kocha wake Ange Postecoglou baada ya siku 40 pekee akiwa amewaongoza katika mechi 8, hakuwa na ushindi wowote katika mechi 10 kuanzia mwanzoni mwa msimu huu.

Hata hivyo, Dyche ambaye alianzia Forest kama mchezaji, alileta mabadiliko ya mara moja, licha ya mabingwa hao mara 2 wa Ulaya kufaidika na maamuzi ya VAR kuwazima mibabe hao wa Ureno.

Morgan Bibbs-White aliwaweka mbele kupitia mkwaju wa penalti baada ya dakika 19 za mchezo, baada Jan Bednarek kuadhibiwa kutokana na handiboli kwenye kijisanduku.

Benadrek hata hivyo alidhani amefuta makosa yake kwa kusawazisha katika kipindi cha kwanza, ila bao lake likafutiliwa mbali na VAR kwa kuotea.

Bao la pili la Forest pia lilifungwa kupitia mkwaju wa penalti baada ya VAR kuingilia.

Huku hayo yakijiri, kocha mkuu wa Aston Villa Unai Emery amesema timu yake ilipewa fundisho kupitia masaibu ya kandanda ya Ulaya baada ya mwanzo wao mwema kutamatika kwa kichapo.

Villa walizabwa mabao 2:1 na Go Aheads wa Uholanzi, licha ya kuanza kwa kishindo mechi yao.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

FOREST YAWAFUNIKA PORTO, VILLA YAFUNZWA

SIKU YA STARLETS UGANI NYAYO

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *