MGOMO WA WAHADHIRI WAKOSA SULUHU
Wanafunzi wa vyuo vikuu vya umma nchini wataendelea kukosa masomo baada ya mazungumzo ya wahadhiri, wizara ya elimu na tume ya kuratibu mishahara ya wafanyakazi wa umm SRC kukosa kuzaa matunda.
Wakati wa kikao kilichoandaliwa katika chuo kikuu cha Machakos, wahadhiri walishinikiza kulipwa shilingi bilioni 7.9 jinsi ilivyo kwenye mkataba wa maelewano wa mwaka 2017-21 na kukataa ofa waliyopewa na serikali.
Wakati uo huo, Waziri wa elimu Julius Ogamba, amesema fedha nyingi zimelipwa kwa awamu na sasa serikali ina deni la shilingi milioni 624 pekee.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































