#Sports

GYOKERES AKATA KIU CHA MAGOLI

Mshambulizi wa klabu ya Arsenal Viktor Gyokeres alifunga mara 2 katika ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Atletico Madrid kwenye mechi ya klabu bingwa barani Ulaya, na kumaliza ukame wake mbele ya lango tangu kuwasili Emirates mwanzoni mwa msimu huu.

Gabriel Magalhaes na Gabriel Martinelli walifungua mvua ya magoli kabla ya Gyokeres kuhakikisha kuwa Arsenal wanapata ushindi katika mechi 3 za ufunguzi bila kufungwa bao.  

Kwa sasa ni Arsenal, mabingwa watetezi PSG na Inter Milan ndizo timu za pekee zenye pointi 9 baada ya mechi 3 za ufunguzi.

Ukame wa Gyokeres umekuwa sehemu ya hofu kwa meneja Mikel Arteta msimu huu, ikizingatiwa kuwa raia huyo wa Uswidi alisainiwa kutoka Sporting Lisbon kunoa makali ya safu ya ushambulizi, akiwa awali amefunga mara 3 pekee katika mechi 11.

Wakati uo huo, Atletico wanasalia bila ushindi ugenini msimu huu.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

GYOKERES AKATA KIU CHA MAGOLI

KENYA YANUSIA KUTETEA UBINGWA ZONE 3

GYOKERES AKATA KIU CHA MAGOLI

HAALAND HASHIKIKI TENA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *