KRU YATAJA VIKOSI VYA SHUJAAS, MORANS
Shirikisho la raga nchini KRU liemzundua rasmi vikosi vya Shujaa na Morans kwa mashindano yam waka huu ya Safari Sevens 2025, yatakayoanza tarehe 10 na kukamilika tarehe 12 mwezi huu katika uwanja wa Nyayo jijini Nairobi.
Mashindano hayo ya kila mwaka yatayashirikisha mataifa kutoka maeneo mbali mbali ya bara la Afrika, Ulaya na pembe zote, Kenya ikilenga kuonyesha ubabe wake katika michezo ya Safari Sevens.
Chini ya uongozi wa kocha mkuu Kevin Wambua, Shujaa inawahusisha wachezaji wakongwe na chipukizi, George Ooro na Samuel Asati wakiwa baadhi ya wachezaji wenye uzoefu kikosini na ambao pia watashirikiana kama manahodha.
Wengine ni Vincent Onyala, Kevin Wekesa na Patrick Odongo, na urejeo wa Christian Ojwang ambaye amekuwa na jeraha kwa kipindi kirefu.
Kikosi cha wanawake kimewajumuisha wachezaji kutoka vikosi vya Kenya Lioness, klabu za hapa nchini, Ubelgiji, Tunisia, Uganda, Costa Blanca Barbarians, Zimbabwe na Shogun.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 










































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































