“MUUAJI” WA IKULU KUZUILIWA KWA SIKU 14
Mshukiwa wa mauaji ya afisa wa GSU nje ya Ikulu ya Nairobi Kithuka Musyimi, atazuiliwa kwa siku 14 zaidi ili kuruhusu polisi kukamilisha uchunguzi katika kifo cha afisa huyo aliyeuawa kwa kudungwa mshale.
Sehemu ya uchunguzi inahusisha ukaguzi wa mienendo ya mshukiwa na mawasiliano ya simu yake, duru zikiarifu kuwa Musyimi na afisa huyo kwa jina Ramadhan Hamisi waliwahi kukutana mara kadhaa kabla ya siku ya tukio.
Hamisi alizikwa nyumbani kwao kaunti ya Kajiado hapo jana.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































