MCHANGO WA BIASHARA NDOGO NA KATI KATIKA UKUAJI WA UCHUMI
Imebainika kuwa Biashara ndogo ndogo na zile za kati, zinahusika pakubwa katika kutoa fursa za ajira kwa wafanyakazi wengi wa Afrika, jambo ambalo ni muhimu katika kufungua sekta isiyo rasmi ya bara.
Idadi ya watu barani Afrika inapoongezeka, benki ziko mbioni kutafuta masoko makubwa zaidi, kwani mara nyingi benki nyingi hupata biashara ili kupanua wigo wao. Kulingana na ripoti ya Mkakati wa Ajira kwa Vijana barani Afrika ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), sekta isiyo rasmi inawakilisha karibu 80% ya nafasi za kazi katika baadhi ya nchi za Afrika.
Upande wa benki nyingi, uwekezaji wa kitamaduni kama vile rehani na hati fungani mara nyingi hupita sekta isiyo rasmi inayostawi barani Afrika, na ndiyo maana baadhi yao sasa wanalenga biashara ndogo na za kati (SMEs).
Imetayarishwa na Maurine Amwayi
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































