#Sports

WANARIADHA WA DEAFLYMPICS WAKAMILISHA WARSHA YA PUFYA

Wanariadha waliochaguliwa kuwakilisha kenya katika mashindano ya riadha ya wanariadha wal;io na changamoto za kusikia yaani Deaflympics jijni Tokyo  mwezi ujao pamoja na voingozi wao wamkamilisha warsha ya siku 4 kuhusu matumizi ya pufya ama dawa za kutitimua misuli.

Warsha hiyo iliyoendeshwa na shirika la kukabiliana na dawa hizo ADAK kwa ushirikiano na wizara ya michezo inalenga kuhakikisha wanariadha wa Kenya wanashindana kwa mujibu wa mwongozo wa riadha katika mashindano hayo.

Aidha baadhi ya wanariadha hao wamesema kuchaguliwa kwao ni fursa muhimu na kusema kuwa wana imani kuwa watashinda na mbali na kutahadhari dhidi ya dawa hizo ili wasipigwe marufuku.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

WANARIADHA WA DEAFLYMPICS WAKAMILISHA WARSHA YA PUFYA

SIKU YA STARLETS UGANI NYAYO

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *