SERIKALI YATANGAZA IJUMAA KUWA HOLIDEI
Serikali imetangaza kesho tarehe 17 kuwa siku ya likizo kwa taifa ili kuwapa wakenya fursa ya kuomboleza kifo cha Waziri mkuu wa zamani Raila Odinga.
Kupitia notisi, Waziri wa usalama wa kitaifa Kipchumba Murkomen amesema hatua hiyo imechukuliwa ili kumuenzi Odinga.
Sherehe za kitaifa kuhusu mazishi ya kitaifa ya Odinga zitafanyika katika uwanja wa Nyayo hapo kesho.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































