ALIYEKUWA WAZIRI MKUU RAILA AFARIKI
Waziri mkuu wa zamani Raila Odinga ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 80.
Kiongozi huyo wa chama cha ODM amefariki mapema leo katika hospitali moja jijini Kochi nchini India, alikokuwa akitibiwa kwa siku 5 zilizopita.
Odinga ambaye amekuwa kiongozi wa upinzani na mbunge wa Lang’ata hadi mwaka 2013, atakumbukwa kwa harakati zake za kuleta mageuzi nchini ikiwemo katiba ya mwaka 2010.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































