IPOA YATAKIWA KUCHUNGUZA VIFO WAKATI WA MSIBA
Mamlaka ya kutathmini utendakazi wa polisi IPOA imetakiwa kuanzisha uchunguzi mara moja kubaini chanzo cha vifo vya watu kadhaa waliofariki wakati wa kuutazama mwili wa Waziri mkuu wa zamani Raila Odinga.
Familia ya Michael Okoth, mkazi wa Kibra mwenye umri wa miaka 23 ambaye mwili wake ulitambuliwa hapo jana, imesema imekuwa ikimsaka mwanao kwa siku 5 baada yake kukosa kurejea kutoka anakofanya kazi.
Kulingana na uchunguzi, alifariki kutoka na kukosa hewa na majeraha kichwani.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































