KNCHR YAONYA KUHUSU KEJELI
Tume ya kitaifa kuhusu haki za kibinadamu KNCHR imewaonya wakenya dhidi ya kuwakejeli watu walio na changamoto za kimaumbile ikiwemo kwenye mitandao ya kijamii, kwamba hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Kulingana na tume hiyo, watakaopatikana na hatia hiyo watatozwa faini ya shilingi milioni 1 au kifungo kischozidi mwaka mmoja au yote mawili.
Onyo ya KNCHR imejiri kufuatia tukio ambao mtu aliye na changamoto za kimaumbile alidhalilishwa mitandaoni maajuzi, tume hiyo ikisema hatua hiyo ni ukiukaji wa katiba na sheria zinawalinda.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































