#Sports

MAPUNGUFU YA FEDHA YATISHIA VIPAJI VYA DEAFLYMPICS

Viongozi wa kikosi cha Kenya kitakachoshiriki mashindano ya Olimpiki kwa wanariadha wasio na uwezo wa kusikia yaani Deaflympics wameweka wazi sababu za kuziacha nje timu saba kwa mashindano hayo yatakayoanza tarehe 15 hadi 26 mwezi Novemba jijini Tokyo.

Awali, Kenya ilikuwa imerataibiwa kushiriki aina 12 za mbio ila ikapunguzwa na kubakia tu kwenye riadha, uogeleaji, mpira wa vikapu kwa wanawake, mpira wa mikono kwa wanaume na gofu.

Timu zilizoondolewa ni ile ya voliboli ya wanawake, soka ya wanawake, mashindano ya baiskeli, tenisi, badminton na mchezo wa bowling

Hata hivyo katika kikao na wahabari, afisa mkuu mtendaji wa Team Kenya Duncan Kuria, amesema uamuzi huo umetokana na mapungufu kwenye bajeti.

Kulingana naye, uzoefu wa kimataifa na namna timu hizo zimekuwa zikifanya vilitumiwa kufanya mchujo wa timu zitakazowakilisha Kenya.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

MAPUNGUFU YA FEDHA YATISHIA VIPAJI VYA DEAFLYMPICS

SHERIA ZA MITANDAO MAHAKAMANI

MAPUNGUFU YA FEDHA YATISHIA VIPAJI VYA DEAFLYMPICS

KENYA YANUSIA KUTETEA UBINGWA ZONE 3

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *