MAHAKAMA KUTOA HATMA YA MASKWOTA KIBOROA
Maskwota wapatao 21,175 walio chini ya muungano wa Kiboroa Squatters Alliance katika kaunti ya Trans Nzoia watafahamu hatma yao ya makazi tarehe 10 mwezi Disemba ambapo mahakama itatoa uamuzi kuhusu kesi waliyowasilisha.
Mahakama ya mazingira na ardhi mjini Kitale ilikamilisha kusikiliza kesi ya maskwota hao hapo jana, maskwota hao wakiitaka mahakama kuwakabidhi sehemu ya ardhi ya shirika la ustawi wa kilimo ADC ili wapate makazi ya kudumu.
Jaji wa mahakama hiyo Christopher Nzili, amewataka wasubiri uamuzi huo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































