MARAGA, MATIANG’I KUUNGANO KABLA YA 2027
Jaji mkuu wa zamani David Maraga na aliyekuwa Waziri wa usalama Fred Matiang’i wamedokeza kuungana katika mrengo mmoja kabla ya uchaguzi mkuu ujao, wakisema hiyo ndiyo njia pekee ya kulihakikishia taifa mageuzi katika uongozi.
Wakizungumza katika hafla 2 tofauti, wawili hao wamesema wataungana na viongozi walio na maono sawa ili kutatua baadhi nya changamoto za nchi.
Aidha, Matiang’i amepuzilia mbali uwepo wa mgawanyiko katika muungano wa upinzani.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































