STARS WAENDELEA KUJIFUA BURUNDI
Timu ya taifa ya Soka Harambee Stars inaendeleza mazoezi yake kabla ya mechi dhidi ya Burundi hapo kesho baada ya kuondoka nchini hapo jana.
Stars ambao tayari walibanduliwa nje ya safari ya kuelekea katika mashindano ya kombe la dunia mwaka ujao, watakuwa wakitumia mechi hiyo kujiimarisha kabla ya mashindano ya ubingwa wa mataifa barani Afrika Afcon.
Mechi yao ya mwisho itakuwa dhidi ya Ivory Coast tarehe 14 mwezi huu, kocha mkuu Benni McCarthy akionya kuonyesha ushindani dhidi ya timu hiyo.
Ushindi dhidi ya Stars utaipa Ivory Coast kufuzu mashindano hayo ya kombe la dunia, ila McCarthy anasema hatatumika kumpa mtu tiketi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































