#Business

SERIKALI YAONDOA ADA ZA KUPATA UPYA VITAMBULISHO ILI KUONGEZA USAJILI WA WAPIGA KURA

Mwananchi sasa ana kila sababu ya kutabasamu baada ya Rais William Ruto kutangaza kuondoa kwa muda ada ya kupata upya vitambulisho vya kitaifa ili kuhakikisha Wakenya wote wanaostahiki wanajiandikisha kama wapiga kura.

Akizungumza katika kaunti ya Vihiga Rais amesema ada hiyo iliyoanzishwa awali ilikuwa na lengo la kudhibiti matumizi mabaya ya huduma hiyo na itasitishwa hadi baada ya uchaguzi.

Ruto pia amefichua mipango ya kuanzisha Hazina ya Miundombinu na Hazina ya Utajiri ili kuharakisha maendeleo ya kitaifa. Hata hivyo, Mfuko wa Miundombinu utafadhili mabadiliko ya kilimo, ujenzi wa viwanda, uzalishaji wa umeme na ujenzi wa barabara, ikiwa ni pamoja na miradi ya vijijini na barabara kuu. 

Imetayarishwa na Maurine Amwayi

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *