WABUNGE WAPENDEKEZA KUPUNGUZWA BEI YA UMEME MARA SITA
Huenda wakenya wakafurahia umeme wa bei nafuu ikiwa pendekezo la Kamati ya Nishati ya Bunge la Kitaifa la kupunguza bei ya jumla ya umeme kwa Ksh9.04 kwa kila kilowati kwa makubaliano mapya ya ununuzi wa umeme litapitishwa. Kwa sasa, baadhi ya kampuni huuza umeme kwa Kenya Power kwa hadi Ksh56 kwa kilowati kila saa, na hivyo kufanya kuwa vigumu kwa msambazaji kupunguza bei ya rejareja bila kupata hasara.
Ripoti inaonyesha kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Kawi David Gikaria amebainisha kuwa pendekezo hilo ni sehemu ya ripoti iliyopatikana baada ya tafiti kutoka nchi zingine-ambayo itawasilishwa Bungeni wakati nchi inajiandaa kuondoa makataa yaliyowekwa tangu 2018.
Imetayarishwa na Maurine Amwayi
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































