KENYA KUOKOA MABILIONI YA PESA KWA KUBADILISHA PESA YA MIKOPO YA SGR
Kenya inatazamiwa kuokoa shilingi bilioni 27.79 kila mwaka baada ya kubadilisha mikopo ya reli ya kiwango cha dola ya Standard Gauge Railway (SGR) kuwa Yuan ya Uchina.
Kama ilivyoripotiwa, Kenya itaanza kulipa kwa sarafu mpya kuanzia Januari mwaka ujao. Waziri wa Hazina ya kitaifa John Mbadi amesema mikopo mingi inayodaiwa na China tayari imebadilishwa, na kuruhusu Kenya kuepuka viwango vya juu vya riba vya dola.
Kenya ilikopa kutoka Benki ya Exim ya China ilifadhili awamu zote mbili za SGR kutoka Mombasa hadi Nairobi na Nairobi hadi Naivasha. Mikopo hiyo, ambayo hapo awali ilihusishwa na viwango vya dola (hadi asilimia 6 ya riba), iliweka Kenya katika hali tete ya sarafu. Hata hivyo, Kenya inakabiliwa na dhiki kubwa ya madeni, huku deni la umma likiwa karibu 70% ya Pato la Taifa, na pia inachunguza njia nyingine za ufadhili.
Imetayarishwa na Maurine Amwayi
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































