GHANA YANUSIA, MISRI YAFUZU KOMBE LA DUNIA
Timu ya taifa ya Ghana iliicharaza Central Africa Republic mabao 5:0 kujiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu kipute cha komb ela dunia mwaka ujao.
Mabao ya Mohammed Salisu, Thomas Partey, Alexander Djiku, Jordan Ayew na Kamaldeen Sulemana, yaliihakikishia Black Stars kusalia kileleni mwa kundi I kwa alama 22, alama 3 mbele ya Madagascar walio katika nafasi ya 2 baada ya mechi 9 kati ya 10.
Ghana watahitaji sare ya aina yoyote katika mechi yao ya mwisho nyumbani dhidi ya Comoros, huku Madagascar wakimaliza kampeni yao ugenini dhidi ya Mali jijini Bamako ambako watalenga kushinda mbali na kuiombea Ghana ianguke.
Timu kutoka shirikisho la CAF ambazo zimefuzu tayari ni, Misri, Tunisia na Morocco.
Misri walifuzu hapo jana baada ya kuitandika Djibouti mabao 3:0, mshambulizi wa Liverpool Mohammed Salah akifunga mabao 2.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































