RUTO, UHURU WAKUTANA NYAYO
Viongozi wakuu nchini na kimataifa wakiongozwa na Rais William Ruto, naibu wake Kithure Kindiki, Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta, jaji mkuu Martha Koome na uongozi wabunge wamejiunga na maelfu ya waombolezaji katika uwanja wa Nyayo ambako ibada ya kitaifa ya mazishi ya Waziri mkuu wa zamani Raila Odinga inaendelea.
Rais Ruto alitangulia kuwaongoza viongozi wengine kuutazama mwili wa Odinga katika majengo ya bunge kabla ya kuelekea Nyayo.
Mwili huo umewasili uwanjani humo dakika chache zilizopita kwenye msafara wa jeshi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































