UGANDA YAKANA KUWATEKA WAKENYA
Kitendawili kimeibuka kuhusu waliko wanaharakati wawili wa Kenya Bob Njagi na Nicholas Oyoo walioripotiwa kutekwa nyara nchini Uganda baada ya idara ya polisi nchini Uganda kukana kuhusika na utekaji nyara wa wawili hao.
Msemaji wa polisi wa Uganda Kituuma Rusoke, amesema hana taarifa kuhusu waliko wanaharakati hao, ambao kulingana na walioshuhudia, walitekwa nyara wiki jana na watu waliokuwa wamejihami kwa bunduki.
Hata hivyo, mawakili nchini wameitaka mahakama itoe amri ya kuishinikiza idara ya jeshi, ile ya ujasusi, inspekta mkuu wa polisi na mwanasheria mkuu wa Uganda wawawasilishe waathiriwa mahakamani.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































