IBADA YA MAZISHI YA ODINGA KUANZA
Ibada ya kitaifa ya mazishi ya waziri mkuu wa zamani Raila Odinga inatarajiwa kuanza muda wowote kuanzia sasa, ikiratibiwa kudumu kwa muda wa saa 2 pekee kuanzia saa tatu asubuhi katika uwanja wa michezo wa Nyayo.
Kwa mujibu wa mwenyekiti mwenza wa kamati ya kitaifa ya mazishi ya Odinga naibu Rais Kithure Kindiki, ibada hiyo pia itahudhuriwa na viongozi wa mataifa na serikali mbali mbali.
Mwili wa Odinga utapelekwa katika kaunti ya Kisumu hapo kesho kabla ya mazishi Jumapili.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































