ODM YAMWITA RUTO AREJEE NYUMBANI
Rais William Ruto atapeperusha bendera ya chama cha ODM kwenye kinyang’anyiro cha urais kwenye uchaguzi mkuu iwapo atakubali kurejea chamani humo.
Haya ni kwa mujibu wa naibu kinara wa ODM Simba Arati, ambaye amemtaja Ruto kama mwaasisi wa chama hicho na hivyo ana nafasi yake chamani.
Kwenye hotuba yake ya Mashujaa hapo jana, Arati ambaye ni gavana Kisii amewataka wanachama kudumisha umoja.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































