#Sports

OWALO ACHUKUA MIKOBA YA ODINGA GOR

Miamba wa soka nchini Gor Mahia wamemteua mkuu wa utendakazi wa serikali kama mlezi wake, na kuchukua mahali pa Waziri mkuu wa zamani Raila Odinga.

Uteuzi wa Owalo umewekwa wazi na mwenyekiti wa Gor Mahia Ambrose Rachier, akisema Owalo anaanza majukumu yake mara moja ili kujaza pengo la Odinga aliyeaga dunia.

Odinga amekuwa mlezi wa Gor Mahia kwa miongo kadhaa, na alichukuliwa kuwa moja kati ya mashabiki sugu wa klabu hiyo.

Owalo amekuwa naibu mlezi wa Gor Mahia tangu mwezi Aprili mwaka huu.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

OWALO ACHUKUA MIKOBA YA ODINGA GOR

MAGAVANA WAMWOMBOLEZA ODINGA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *