#Sports

TUNISIA YAWEKA HISTORIA SAFARINI KUELEKEA KOMBE LA DUNIA

Timu ya taifa ya Tunisia ilihitimisha kampeni yake ya kusaka tiketi ya kushiriki kombe la dunia mwaka ujao bila kufungwa bao walipoicharaza Namibia mabao 3:0 kwenye mechi yao ya mwisho ya kundi H hapo jana.

Tunisia walimaliza kampeni yao kwa kushinda mechi 9 kati ya 10, wakifunga mabao 22 kushiriki fainali hizo.

Bao la kwanza kupitia mkwaju wa penalti lake Ali El Abdi katika kipindi cha kwanza lilifuatwa na lake Hannibal Mejbri na nahodha Ferjani Sassi katika kipindi cha pili.

Namibia kwa upande wao walimaliza wa pili kwenye kundi licha ya kichapo hicho, wakiwa wamemaliza katika nafasi hiyo katika kampeni 3 zilizopita, ila alama zao 15 hazitawawezesha kushiriki mwondoano wa timu 4 zitakazomaliza kama nambari 2 bora.

Liberia walimaliza wa 3 baada ya sare ya bao 1 dhidi ya Equatorial Guinea iliyochezesha kikosi baada ya kumtimua kocha mkuu na wachezaji kadhaa mahiri kufuatia hatua yao ya kudinda kusafiri nchini Malawi kwa mechi mwishoni mwa wiki jana.

Kampeni hiyo itakamilika hii leo wakati ambapo jumla ya mechi 11 zitachezwa.

Harambee Stars wa Kenya watavaana na wenyeji Ivory Coast ambao wanaongoza kundi F kwa pointi 23, Gabon walio katika nafasi ya pili wakichuana na Burundi nyumbani.

Kizaazaa kinatarajiwa katika kundi C wakati Afrika Kusini watalenga kupata ushindi dhidi ya Rwanda, nao Benin wakichuana na Nigeria, Afrika Kusini, Benin na Nigeria wote wakiwania nafasi ya kwanza.

Tayari timu 6 ambazo ni Cape Verde, Algeria, Ghana, Misri, Tunisia na Morocco zimefuzu, nafasi 3 za moja kwa moja zikitarajiwa kujazwa hii leo.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

TUNISIA YAWEKA HISTORIA SAFARINI KUELEKEA KOMBE LA DUNIA

CAPE VERDE YAFUZU KOMBE LA DUNIA MBELE

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *