MEMPHIS DEPAY AIBIWA PASPOTI BRAZIL
Huku taifa la Uholanzi likilenga kuzidisha uongozi wa kundi G katika kinyang’anyiro cha kufuzu mashindano ya kombe la dunia mwaka ujao, hofu imeibuka kuhusu uwepo wa nyota wao mahiri Memphis Depay ambaye ameripoti kwamba paspoti yake iliibiwa nchini Brazil.
Depay anayeichezea klabu ya Corinthians nchini Brazil, alikuwa ameratibiwa kusafiri Jumapili kujiunga na wenzake wa timu ya taifa katika maandalizi ya pambano dhidi ya Malta na Finland akalazimika kuchelewa.
Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United, ndiye mfungaji bora zaidi wa magoli nchini Uholanzi akiwa na mabao 52 katika mechi 104, baada ya kuvunja rekodi ya Robin van Persie mwezi jana.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































