SERIKALI KUANZISHA USHURU MPYA WA MAFUTA, UMEME
Wakenya katika siku zijazo huenda wakalazimika kulipa ushuru mpya wa mafuta na umeme huku serikali ikichukua hatua ya kuanzisha Hazina ya Kawi Shirikishi (CEF) ili kufadhili miradi muhimu ya kawi na kupunguza utegemezi wa mikopo.
Kulingana na Waziri wa kawi Opiyo Wandayi, hazina hiyo itachukua michango kutoka kwa wadau wa sekta ya nishati pamoja na mgao wa Bunge, dhamana za serikali, mali iliyorejeshwa, na faini kutoka kwa Mamlaka ya Kudhibiti Kawi na Petroli (EPRA).
Kulingana na ripoti hii inaweza pia kujumuisha kuanzishwa kwa ushuru mpya wa mafuta na umeme.Kwa sasa, wakenya tayari wanalipa ushuru kadhaa unaohusiana na nishati, ikiwa ni pamoja na Ushuru wa Matengenezo ya Barabara (Ksh25 kwa lita ya petroli na dizeli), Ushuru wa Maendeleo ya Petroli (Kshh5.40 kwa lita), na Ushuru wa Umeme Vijijini (5% ya matumizi ya nishati).
Imetayarishwa na Maurine Amwayi
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































