#Sports

POLICE FC KUCHEZA BILA MASHABIKI, WANAHABARI

Mechi ya raundi ya pili ya kuwania ubingwa wa klabu bingwa barani Afrika CAF kati ya Police FC ya Kenya na Al-Hilal ya Sudan hii leo imehamishwa kutoka uwanja wa Kasarani hadi ule wa Ulinzi Complex.

Kwa mujibu wa shirikisho la soka nchini FKF, uhamisho huo umetokana na ibada ya kitaifa ya mazishi ya Waziri mkuu wa zamani Raila Odinga, na kwamba mechi hiyo itaendelea kama ilivyopangwa na wala haitasitishwa ilivyo kwa mechi za FKF.

Hata hivyo, shirikisho la soka barani Afrika CAF limesema mechi hiyo itachezwa bila mashabiki wala wanahabari.

Huku hayo yakijiri, mechi baina ya mashirikisho yaliyo chini ya CAF yaani CAF Confederations kati ya Nairobi United na Etoile Sportive du Sahel ya Tunisia itasakatwa Jumapili katika uwanja wa Ulinzi Sports Complex.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

POLICE FC KUCHEZA BILA MASHABIKI, WANAHABARI

OWALO ACHUKUA MIKOBA YA ODINGA GOR

POLICE FC KUCHEZA BILA MASHABIKI, WANAHABARI

EPL KUREJEA ARSENAL WAKIPATA PIGO

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *