UPINZANI: KALONZO HAJI
Viongozi wa mrengo wa upinzani wamekariri kuwa kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka hayuko tayari kujiunga na serikali ya Kenya Kwanza, wakiitaka serikali kusitisha juhudi za kumrai ajiunge nayo.
Wakiongozwa na aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua, Martha Karua wa PLP na Eugene Wamalwa wa DAP-K baada ya kujiunga na Musyoka kwenye ziara ya Ukambani, viongozi hao wamewahimiza vijana kusajiliwa kwa wingi kama wapiga kura.
Wanasema hiyo ndiyo njia mwafaka ya kupata mageuzi nchini.
Imeatayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































