KIJANA MMOJA AFARIKI WAKATI WA USAJILI WA MAKURUTU
Kijana mmoja mwenye umri wa miaka ishirini na miwili ameripotiwa kufariki wakati wa zoezi la usajili wa makurutu wa kujiunga na jeshi katika eneo la chwele, kaunti ndogo ya kabuchai.
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi wa bungoma, David saina, kijana huyo, ambaye alikuwa mwanafunzi wa chuo kikuu cha masinde muliro huko kakamega, alizirai wakati wa tathmini ya udhibiti wa mwili na alithibitishwa kufariki alipofikishwa hospitalini.
Imetayarishwa na Jones Koikai
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































