UTEKAJI: RUTO ATAKIWA KUINGILIA KATI
Familia ya mwanaharakati Nicholas Oyoo aliyeripotiwa kutekwa nyara nchini Uganda akiwa na mwenzake Bob Njagi imemtaka Rais William Ruto sasa kushauriana na mwenzake wa Uganda Yoweri Museveni ili kufanikisha kupatikana kwa wanaharakati hao.
Wawili hao wametoweka kwa siku 12 sasa bila kujulikana waliko, wanaharakati wenza nchini wakitishia kufanya maandamano kote nchini siku ya Alhamisi iwapo hawatakuwa wamepatikana.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































