MASWALI KUHUSU MALIPO YA 77M KUSAKA 13M NHIF
Kamati ya uhasibu wa umma katika bunge la seneti imeibua hofu kuhusu malipo ya juu yaliyotolewa kwa mawakili katika bima ya zamani NHIF katika kipindi cha mwaka wa kifedha wa 2020-21, shilingi milioni 77 zikiripotiwa kutolewa katika kesi ya kurejesha shilingi milioni 13.
Hofu hiyo iliibuliwa kwenye kikao na afisa mkuu mtendaji wa mamlaka ya SHA Dakta Mercy Mwangangi, akiwaahidi maseneta kwamba atatoa majibu kuhusu maswali yao ndani ya muda wa wiki 3.
Licha ya kutaka kujiondoa, maseneta wamesisitiza kwamba anafaa kuwajibikia ubadhirifu huo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 








































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































