DENI KUATHIRI MASOMO YA GREDI YA 10
Huenda masomo ya wanafunzi wa gredi ya 10 mwaka ujao yakatatizika kutokana na ukosefu wa vitabu, ambavyo wachapishaji wanasema hawajachapisha hadi sasa kutokana na deni la shilingi bilioni 11.4 wanalodai serikali.
Kupitia kwa muungano wao, wachapishaji wamesema deni hili litaathiri uchapishaji na usambazaji wa vitabu hivyo, wakiitaka serikali kulipa deni hilo.
Nakala milioni 7 za vitabu hivyo zimeratibiwa kuchapishwa, zoezi wanalosema huchukua miezi 2 huku usambazaji ukichukua mwezi mmoja.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































