KMPDU YATAKA KIAMBU IVUNJILIWE MBALI
Mgomo wa madaktari katika kaunti ya Kiambu umendelea kuibua maswali kuhusu uwezo wa serikali za kaunti kushughulikia masuala ya afya, madaktari kwenye kaunti hiyo wakisitisha huduma zao zote na kuanzisha mchakato wa kumtaka Rais William Ruto kuvunjilia mbali serikali ya kaunti hiyo.
Kupitia muungano wao KMPDU, madaktari wameishutumu serikali ya kaunti ya Kiambu kwa madai ya kuingiza siasa katika suala la afya, huku mgomo huo ukigonga siku ya 139.
Hata hivyo, Waziri wa afya Aden Duale ametoa wito kwa mgomo huo kutatuliwa mara moja.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































