ZANU-PF KUONGEZA MUHULA WA RAIS MNANGAGWA
Mrengo wa Upinzani nchini Zimbabwe umepinga pendekezo la chama tawala ZANU-PF kuifanyia marekebisho katiba ili kuongeza muhula wa rais Emerson Mnangagwa kwa kipindi cha miaka 2.
Pendekezo hilo liliafikiwa Jumamosi iliyopita kwenye kongamano la chama hicho, na iwapo litapitishwa, Mnangagwa mwenye umri wa miaka 83 ataongoza hadi mwaka wa 2030.
Hata hivyo, mojawapo wa viongozi wa upinzani James Timba, amesema Zimbabwe haifai kuongozwa na maazimio yanayotokana na makangamano ya kisiasa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































