KENYA YANUSIA KUTETEA UBINGWA ZONE 3
Juhudi za Kenya kutetea ubingwa wa masumbwi wa Africa Zone 3 zimepigwa jeki baada ya Faith Nafuna kujihakikishia nafasi katika fainali za pambano la Flyweight kwa wanawake hapo jana.
Nafuna alimbwaga mwenzake wa Tanzania Sarafina James Fusi katika pambano kali la semi fainali ugani Kasarani jijini Nairobi, na atashiriki fainali Ijumaa wiki hii.
Akizungumza baada ya ushindi huo, mwanamasumbwi huyo ameelezea matumaini ya kutetea ubingwa wan chi, hasa kutokana na ukakamavu uliohitajika kabla ya kufuzu fainali.
Kauli yake ikisisitizwa na kocha wa kitaifa wa timu ya masumbwi John Ochieng.
Katika pambano tofauti la Flyweight, mwanamasumbwi wa DR Congo Nyembo Muamba Giselle alifuzu fainali baada ya kumzidi mwenzake wa Uganda Angela Katushabe.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































