KCSE KUANZA LEO
Jumla ya watahiniwa elfu 990 wa mtihani wa kitaifa wa kidato cha 4 KCSE wameratibiwa kuanza mtihani huo hii leo na kukamilika tarehe 21 mwezi ujao.
Kwa mujibu wa ratiba ya baraza la mitihani ya kitaifa KNEC, mitihani ya Kifaransa, Kijerumani, lugha na ishara inaanza hii leo na kufuatiwa na mitihani ya utendaji yaani practical ambayo itaanza hapo kesho hadi tarehe 31 mwezi huu.
Mitihani ya nadharia ama theory, itaanza tarehe 3 mwezi ujao, somo la Fizikia likifunga ratiba hiyo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































