MVUA KUBWA KUANZA LEO, IDARA YAONYA
Umetakiwa kuchukua tahadhari kuhusu mvua kubwa katika maeneo mbali mbali kuanzia leo, ambao ndio mwanzo wa kipindi kifupi cha mvua ya Oktoba- Novemba kuelekea Disemba.
Katika taarifa, idara ya utabiri wa hali ya anga imesema mvua inayoshuhudiwa katika maeneo ya Ziwa Victoria, Rift Valley, nyanda za juu za Magharibi mwa Rift valley inatarajiwa kuonhezeka ndani ya saa 24 na kuenea katika maeneo yaliyo Mashariki mwa Rift Valley, ikiwemo Nairobi.
Imeongeza kuwa mvua hiyo itaendelea kwa siku kadhaa zijazo, na kusambaa katika maeneo ya Kaskazini Mashariki ya nchi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 










































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































