MWONDOANO WA CAF KUCHEZWA MOROCCO
Shirikisho la soka barani Afrika CAF limetangaza kwamba mashindano ya mwondoano kwa timu 4 zitakazomaliza katika nafasi ya pili bora kutoka makundi yote 9 kwenye kinyang’anyiro cha kufuzu kombe la dunia yaani playoff yataandaliwa nchini Morocco kuanzia tarehe 13 hadi 16 mwezi ujao.
Mshindi wa mashindano hayo atashiriki awamu ya mwondoano ya mabara ili kusaka tiketi ya kufuzu kombe hilo litakaloandaliwa katika mataifa ya MArekani, Mexico na Canada.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 








































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































