MUSYOKA AKATIZA ZIARA UINGEREZA, AREJEA
Aliyekuwa makamu wa rais Kalonzo Musyoka ambaye ni kinara wa Wiper, amelazimika kukatiza ziara yake ya siku 10 nchini Uingereza na kurejea nchini mapema leo kutokana na kifo cha Waziri mkuu wa zamani Raila Odinga.
Akiwahutubia wanahabari baada ya kuwasili katika uwanja wa JKIA, Musyoka ameeleza kushtushwa na kifo cha Odinga, ambaye amekuwa mshirika wake wa kisiasa kwa miaka mingi na kwamba bado hajaamini kwamba Odinga amefariki.
Musyoka alikuwa ameratibiwa kuhutubia kongamano la kisiasa na tuzo la London katika bunge la Uingereza, mbali na kutoa mihadhara katika chuo kikuu cha Oxford.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































