#Local News

RUTO ATETEA SHERIA ZA MITANDAO

Rais William Ruto ametetea sheria za kudhibiti utumizi wa mitandao ya kijamii alizoidhinisha, akiwaonya wakenya anaosema wanaeneza uvumi kuhusu sheria hizo.

Kulingana na Rais, sheria hizo zinalenga kudhibiti ugaidi, mahubiri potovu na ukiukaji wa maadili ya jamii, huku akijitetea kutokana na uamuzi wake wa kutia Saini sheria hizo wakati taifa lilikuwa kwenye maombolezo ya Waziri mkuu wa zamani Raila Odinga.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *