#Sports

GOR WATAMBA, KCB YATAPA

Miamba wa soka nchini Gor Mahia wamejihakikishia ushindi katika mechi mbili mfululizo katika Liugi kuu KPL, baada ya kuipokeza KCB FC yake Robert Matano kichapo cha bao 1:0 katika uwanja wa Dandora hapo jana.

Bao la pekee la mchezo huo lilipachikwa wavuni na Felix Mboya, na kuipa Gora lama 3 muhimu ambao sasa zimewaweka katika nafasi ya tatu kwa alama 6 sawa na KCB, na alama 3 nyuma ya Vigogo Shabana FC ambao walitoa sare ya bao 1 dhidi ya Tusker FC.

Licha ya kuanza msimu kwa ushindi wa mabao 2:0 dhidi ya Tusker FC, kichapo cha hapo jana kinamaanisha sasa Matano amepoteza mechi 2 baada ya mechi 4.

Katika mechi nyingine, bingwa mtetezi Police FC na Mara Sugar walijipatia ushindi wa kwanza wa msimu, huku limbukeni APS Bomet wakiendelea kukaribishwa kwa kipigo katika ligi kuu nchini.

Clinton Kinanga aliifungia Police FC bao la pekee kwenye debi ya maafande katika uwanja wa Kericho Green Stadium, kichapo hicho kikimaanisha kwa APS wamepoteza mech izote 3 za mwanzo wa msimu wao wa kwanza katika ligi kuu.

Katika mechi za leo, Nairobi United watashuka dimbani dhidi ya Bidco United katika kaunti ya Murang’a majira ya 3PM.

Imetayarishwa na Nelson Andati

GOR WATAMBA, KCB YATAPA

MOMBASA UNITED WAONYESHA MAKALI NSL

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *