GAVANA KAHIGA AJIUZULU
Gavana Nyeri Mutahi Kahiga amejiuzulu kutoka wadhifa wa mwenyekiti wa baraza la magavana kutokana na shutuma dhidi yake kuhusiana na kauli zake zinazoonekana kusherehekea kifo cha Waziri mkuu wa zamani Raila Odinga.
Kupitia taarifa, Kahiga amejutia kauli zake na kuomba msamaha kwa familia ya Odinga, chama cha ODM, magavana wenzake na jamii ya eneo zima la Nyanza kabla ya kuwasilisha barua ya kujiuzulu.
Aidha, amekariri kuwa kauli hizo ulikuwa msimamo wake binafsi na wala si wa wakazi wa Nyeri.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































