HOFU YA USALAMA YAKUMBA MECHI ZA ISRAEL
Hofu ya kiusalama imeendelea kukumba mechi za timu ya taifa ya Israel dhidi ya Norway na Italia, mayor wa jimbo la Udine lililoko kaskazini mwa Italia akionya kuhusu hali ya usalama mechi hiyo inapoandaliwa wiki ijayo.
Israel itasafiri kuelekea Norway kwa mechi ya Jumamosi, kabla ya kumenyana na Italia Jumanne katika mechi za kundi I, mechi ambayo idadi ya mashabiki imedhibitiwa.
Katika wiki za hivi karibuni, waandamanaji wamekuwa wakifurika barabarani nchini Italia kuhusiana na uvamizi wa Israel dhidi ya Gaza.
Makabiliano yamekuwa yakishuhudiwa baina ya polisi na waandamanaji katika miji kama vile Rome na Milan.
Mayor wa jimbo la Udime Alberto Felice de Toni, aliwaambia wanahabari kwamba alipendelea mechi hiyo kuahirishwa kutokana na hofu hiyo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































