#Sports

KYLLIAN MBAPPE YUKO SAWA, DESCHAMPS

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ufaransa Didier Deschamps amethibitisha kuwa mshambulizi matata wa timu hiyo na klabu ya Real Madrid Kylian Mbape yuko sawa kushiriki mechi ya kuwania kufuzu katika kombe ka dunia litakaloandaliwa mwaka ujao.

Mbappe ambaye amekuwa tegemeo kwa Les Blues msimu huu, aliondoka uwanjani akichechemea mwishoni mwa mechi kati ya Real Madrid na Villareal na nafasi yake kujazwa na Rodrygo.

Kulingana na jarida la L’Equipe nchini Ufaransa, Mbappe alipata jeraha dogo la muundi wa mguu kwenye mechi hiyo, ila Deschamps amesisitiza kuwa fowadi huyo yuko sawa.

Ufaransa ambao wanaongoza kundi D, watamenyana na Azerbaijan nyumbani Ijumaa kabla ya kusafiri kuelekea Iceland Jumatatu, na iwapo watashinda mechi hizo mbili basi watajikatia tiketi ya kufuzu mashindano ya kombe hilo.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

KYLLIAN MBAPPE YUKO SAWA, DESCHAMPS

STARS MBIONI KUREJESHA NYOTA

KYLLIAN MBAPPE YUKO SAWA, DESCHAMPS

MEMPHIS DEPAY AIBIWA PASPOTI BRAZIL

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *