UPDF YAKANA KUWAZUILIA NJAGI, OYOO
Utata umeendelea kuibuka kuhusu waliko wanaharakati Bob Njagi na Nicholas Oyoo baada ya jeshi la ulinzi la Uganda UPDF kukana kuwazuilia wawili hao walioripotiwa kutekwa nyara nchini Uganda yapata mwezi mmoja uliopita.
Kwenye taarifa yake kwa mahakama, UPDF imesema kwamba imeendesha uchunguzi na msako katika vituo vyote vya kuwazuilia washukiwa ila hakuna taarifa kuhusu wawili hao.
Hii ni baada ya jeshi hilo kuamriwa na mahakama kutoa taarifa kuhusu waliko wawili hao katika kesi iliyowasilishwa mahakamani na mawakili nchini humo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































