NAIROBI UNITED WAZIDI KUANGUSHA MIAMBA
Klabu ya Nairobi United inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini KPL imeendelea kuvunja vizuizi na kujitangaza katika majukwaa ya kimataifa, baada ya kupata ushindi muhimu wa mabao 2:0 nyumbani dhidi ya Etoile Sportive du Sahel ya Tunisia katika mkondo wa kwanza wa awamu ya mwisho ya mwondoano wa mechi za mashirikisho ya bara yaani CAF Confederations Cup.
Kwenye mechi iliyochezwa katika uwanja wa Ulinzi Complex jijini Nairobi, Wing’a wa zamani wa AFC Leopards na Kariobangi Sharks Ovella Ochieng aliwaweka Naibois kifua mbele katika dakika ya 37, ya kuchangia bao la pili baada ya du Sahel kushindwa kuondoa mpira kutokana na kona.
Kabla ya mechi hiyo, kulishuhudiwa kimya cha dakika moja kutoa heshima kwa Waziri mkuu wa zamani Raila Odinga ambaye taifa linaendelea kumwomboleza.
Etoile Sportive ambao wanajivunia beki wa zamani wa Gor Mahia Alphonce Omija, walianza mechi hiyo kwa kishindo ila wakadhibitiwa na safu imara ya ulinzi ya Nairobi United.
Mkondo wa 2 wa mechi hiyo utachezwa nchini Tunisia Jumapili ijayo. Mshindi akifuzu kuingia awamu ya makundi.
Wakati uo huo, Miamba wa soka barani Afrika Pyramids ndio mabingwa wa taji la CAF Super Cup kwa mara ya kwanza baada ya kuinyuga RS Berkane wa Morocco bao 1:0 kwenye fainali za taji hilo zilizoandaliwa kwenye uga wa 30 June jijini Cairo.
Bao la pekee la mchezo lilifungwa na mshambulizi wa timu ya taifa ya DR Congo Fiston Mayele baada ya kuandaliwa pasi na beki wa timu ya taifa ya Morocco Mohammed Chibi kunako dakika ya 75.
Taji la CAF Super Cup huwakutanisha mabingwa wa kombe la klabu bingwa barani Afrika na mabingwa wa taji la mashirikisho la CAF.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































