NIPO UNITED, BRUNO FERNANDES
Kiungo wa klabu ya Manchester United Bruno Fernandes ameweka wazi kwamba hana nia ya kuhamia ligi ya Saudi Pro mwishoni mwa msimu ujao, na badala yake analenga kusalia United.
Duru zilizo karibu na mchezaji huyo wa Ureno zimesema kwamba alikatalia mbali ofa kutoka kwa klabu za Al-Hilal na Al-Ittihad mwishoni mwa msimu jana, ili kuendelea kutumika Old Trafford.
Kwa mujibu wa shirika la Uingereza la BBC, nia ya Fernandes ambaye kandarasi yake inakamilika mwaka wa 2027 akiwa na uwezo wa kuongeza mwaka mmoja, ni kuendelea kucheza katika ligi kuu za bara Ulaya.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































