#Sports

FKF YAFUTILIA MBALI LIGI KWA SIKU 7

Shirikisho la soka nchini FKF limefutilia mbali ratiba za mechi zote za ligi nchini wakati wa kipindi cha siku 7 za maombolezo ili kumuenzi Waziri mkuu wa zamani Raila Odinga.

Kupitia taarifa, katibu mkuu wa FKF Harold Ndege amesema kuwa mecho zote za ligi kuu KPL, NSL kwa wanaume kwa wanawake na zile za mashinani ziliokuwa zimeratibiwa katika kipindi hicho zimesitishwa hadi maombolezo yakamilike.

Odinga ambaye amekuwa shabiki wa siku zote wa kandanda ya humu nchini, alichukuliwa kuwa watu wenye ushawishi mkubwa waliotetea maslahi ya spoti.

Hadi kifo chake, Odinga amekuwa kinara wa klabu ya Gor Mahia inayoshiriki ligi kuu nchini, na shabiki wa timu ya taifa Harambee Stars na klabu ya Arsenal inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Uingereza.

Kifo chake ni pigo kwa Gor Mahia, ambayo wiki chache zilizopita, alikuwa ameahidi kuipa msaada wa shilingi milioni 10 ili lufanikisha shughuli za klabu hiyo katika msimu unaoendelea wa 2025-26.

FKF imesema itatangaza ratiba mpya kwa mechi zitakazoathirika na kipindi cha maombolezo.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

FKF YAFUTILIA MBALI LIGI KWA SIKU 7

WAKENYA WAMIMINIKA JKIA

FKF YAFUTILIA MBALI LIGI KWA SIKU 7

STARLETS WAJIANDAA KWA WAFCON

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *